Riyadh, Saudi Arabia
Klabu ya Al Ahli ya Saudi Arabia inadaiwa kujiandaa kumnunua winga wa Man City, Riyad Mahrez (pichani) kwa ada inayotajwa kufikia Pauni 30 milioni.
Habari za ndani zinadai kwamba kocha wa Man City, Pep Guardiola anajiandaa kufanya mazungumzo na Mahrez huku suala la ofa ya Saudi Arabia kwa mchezaji huyo likitarajiwa kutawala mjadala huo.
Mahrez ambaye pia ni nyota wa timu ya Taifa ya Algeria, mwenye umri wa miaka 32 anadaiwa kuwa tayari kuchangamkia ofa hiyo licha ya umuhimu alionao katika kikosi cha Man City lakini zipo habari kwamba amekuwa akitaka nyongeza ya mshahara.
Klabu ya Al Ahli katika mkakati wa kumpata Mahrez inadaiwa kumtengea Pauni 865,000 kwa wiki na mchezaji huyo ambaye amebakiwa na miaka miwili katika mkataba wake na Man City wenye thamani inayotajwa kufikia Pauni 6 milioni.
Katika msimu uliopita wa 2022-23 ambao Man City imeweka rekodi kwa kubeba mataji matatu kuanzia Ligi Kuu England (EPL) FA na Ligi ya Mabingwa Ulaya, Mahrez ameifungia timu hiyo mabao 10 katika mechi 41.
Wakati mpango wa Mahrez ukiwa hatua za awali, mchezaji mwingine ambaye huenda akaelekea Saudi Arabia ni nahodha wa Liverpool, Jordan Henderson ambaye amepewa ofa ya Pauni 700,000 kwa wiki ili kujiunga na timu ya Al-Ittifaq inayonolewa na nahodha wa zamani wa Liverpool, Steven Gerrard.
Kimataifa Mahrez naye Saudi Arabia kunamhusu
Mahrez naye Saudi Arabia kunamhusu
Read also
