Na mwandishi wetu
Mtibwa Sugar imesema inahitaji ushindi katika mechi zake 10 zijazo ili kubaki salama kwenye Ligi Kuu NBC.
Timu hiyo inayoshika mkia kwa pointi 16 haikuwa na mwenendo mzuri katika michezo kadhaa iliyopita, ila sasa imeanza kurejesha matumaini.
Katika michezo 20 iliyocheza imeshinda minne pekee na miongoni walizoshinda ni michezo ya hivi karibuni dhidi ya Tanzania Prisons kwa ushindi wa mabao 2-1 na dhidi ya Singida FG mabao 2-0 huku wakitoka sare tasa dhidi ya Kagera Sugar.
Ofisa Habari wa Mtibwa, Thobias Kifaru (pchani) alisema matokeo ya mechi hizo zilizopita yanawapa matumaini makubwa kuwa wameanza kurejea na sasa wanachotizama na namna ya kushinda michezo 10 iliyobaki.
Kifaru alisema timu itarejea kambini kuanzia keshokutwa Ijumaa kujiweka imara na kujiandaa kwanza na mchezo wa Kombe la ASFC raundi ya nne dhidi ya Azam FC utakaochezwa April 7, mwaka huu.
Soka Mtibwa yasaka ushindi mechi 10
Mtibwa yasaka ushindi mechi 10
Read also