Na mwandishi wetu
Azam FC imeaga rasmi michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika katika hatua ya awali ikitolewa kwa mikwaju ya penalti 4-3 na Bahir Kenema ya Ethiopia baada ya kupata ushindi wa mabao 2-1.
Ikiwa kwenye uwanja wake wa nyumbani wa Azam Complex, Chamazi jijini Dar es Salaam Ijumaa hii, Azam FC ilipambana na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 na kufanya matokeo ya jumla yawe sare ya jumla 3-3.
Katika mechi ya kwanza ambayo Kenema FC walikuwa wenyeji, timu hiyo pia ilipata ushindi wa mabao 2-1 na Azam FC kujipa matumaini ya kulipa kisasi lakini mwisho wa siku ikaishia kupata matokeo ambayo yalizipeleka timu hizo kwenye mikwaju ya penalti na Azam FC kushindwa kutamba.
Kwa matokeo hayo, Azam FC sasa itaanza kupambana upya kusaka tiketi ya ushiriki wa michuano ya Afrika msimu ujao kupitia Ligi Kuu NBC pamoja na michuano ya kuwania Kombe la FA.
Kutolewa kwa Azam FC kunazifanya timu za Ligi Kuu NBC zinazoshiriki michuano ya klabu barani Afrika kubaki tatu ambazo ni Simba na Yanga zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa na Singida Fountain Gate inayoshiriki Kombe la Shirikisho.
Soka Azam FC yaaga mapema
Azam FC yaaga mapema
Read also