Munich, Ujerumani
Bayern Munich imewataka mabosi wa Tottenham Hotspur wawe hadi leo Ijumaa wameamua kama wanajiandaa kumuuza mshambuliaji wao na nahodha wa England Harry Kane.
Hatma ya Kane katika kikosi cha Spurs imekuwa mjadala kwa siku za karibuni baada ya klabu kadhaa kubwa barani Ulaya kumtaka huku mwenyewe akidai kwamba angependa zaidi kujiunga na Bayern.
Bayern tayari imeshawasilisha ofa ya kumtaka Kane ambaye kwa mujibu wa chanzo kimoja cha habari nchini Ujerumani, mchezaji huyo amekubali ofa hiyo ingawa mabosi wake wanasita kutoa uamuzi.
Kitendo cha mabosi wa Bayern kutaka jibu kuhusu mchezaji huyo ni ishara ya kukerwa na mazingira ya yaliyogubila usajili wa mchezaji huyo na haitokuwa ajabu wakiamua kuachana naye kama Spurs haitowapa jibu la uhakika.
Kane ambaye ametimiza miaka 30, ndiye mfungaji wa mabao wa wakati wote Spurs na ana mwaka mmoja katika mkataba wake na timu hiyo, licha ya Bayern kuonekana kumtaka hadi kutaka ipewe jibu lakini mabosi Spurs hawajatoa jibu lolote hadi sasa.
Mchezaji huyo pia hayupo tayari kuongeza mkataba na Spurs na kama klabu hiyo haitompiga bei wakati huu ijiandae kumuona akiondoka msimu ujao akiwa huru na wao kutovuna chochote kwa mkali huyo wa kuzifumania nyavu.
Mwenyekiti wa Spurs, Daniel Levy na maofisa waandamizi wa Bayern walikutana hivi karibuni lakini hakuna makubaliano yaliyofikiwa licha ya mmiliki mwenye hisa nyingi katika klabu hiyo, Joe Lewis kunukuliwa siku chache zilizopita akitaka Kane auzwe.
Kimataifa Bayern wataka Spurs itoe jibu kuhusu Kane
Bayern wataka Spurs itoe jibu kuhusu Kane
Read also