Na mwandishi wetu
Nyota mpya wa Simba, Saleh Kabaraka (pichani) ameanza na mguu mzuri katika kikosi cha timu yake hiyo mpya baada ya kufunga bao wakati Simba ikiilaza JKU mabao 3-1 katika mechi ya Kombe la Mapinduzi.
Mechi hiyo iliyopigwa leo Jumatatu Amaan Complex mjini Unguja, ni ya kwanza kwa Kabaraka kucheza akiwa na jezi ya Simba ikiwa ni muda mfupi tangu usajili wake utangazwe rasmi na klabu hiyo.
Kabaraka amejiunga na Simba akitokea JKU, ni mmoja wa wachezaji mahiri waliong’ara msimu uliopita akiwa na rekodi ya mabao zaidi ya 20, anajiunga na Simba inayoshiriki Ligi Kuu NBC lakini pia ina mtihani wa Ligi ya Mabingwa Afrika ikiwa hatua ya makundi.
Mbali na Kabaraka, mabao mengine mawili ya Simba yalifungwa na Moses Phiri na Jean Baleke wakati bao pekee la JKU lilifungwa na Nova Kaboma.
Matokeo hayo yanaifanya JKU kuaga rasmi michuano ya Kombe la Mapinduzi msimu huu wa 2023-24 ikiwa imepoteza mechi ya pili kwani kabla ya hapo ililala mbele ya Singida Fountain Gate.
Baada ya mechi hiyo ambayo imeipa Simba ushindi wa kwanza kwa mwaka 2024, beki tegemeo wa kati wa Simba, Che Malone Fondoh alitangazwa kuwa mchezaji bora wa mechi hiyo.
Katika mechi nyingine ya michuano hiyo, Singida Fountain Gate iliichapa APR mabao 3-1, huku mabao ya Singida FG yakifungwa na Rupiya Elvis, MOrrice Chukwu na Fancy Kazadi wakati bao pekee la APR lilifungwa na Mbaoma Victor.
Soka Kabaraka aanza vizuri Simba, JKU yalala 3-1
Kabaraka aanza vizuri Simba, JKU yalala 3-1
Related posts
Read also
