Milan, Italia
Kiungo wa Newcastle na timu ya taifa ya Italia, Sandro Tonali (pichani) amefungiwa kucheza soka kwa kipindi cha miezi 10 na Shirikisho la Soka Italia (FIGC) kwa kosa la kujihusisha na uchezaji kamari.
Adhabu hiyo inamfanya mchezaji huyo asiruhusiwe kucheza soka hadi Agosti mwakani na kwa maana hiyo atazikosa fainali za Kombe la Ulaya 2024 au Euro 2024 Juni mwakani kama Italia itafuzu.
Tonali alijiunga na Newcastle Julai mwaka huu kwa ada ya Pauni 55 milioni huku kukiwa na matarajio makubwa kwake kuibeba vyema timu hiyo katika Ligi Kuu England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Taarifa ya FIGC ilithibitisha kufungiwa kwa mchezaji huyo na kufafanua kwamba amevunja kanuni inayowakataza wachezaji kucheza kamari katika mechi za soka zinazoandaliwa na FIGC, Uefa na Fifa na mbali na adhabu hiyo, mchezaji huyo pia ametozwa faini ya Pauni 17,380.
Adhabu ya aina hiyo ni ya pili kutolewa katika siku za karibuni baada ya mapema mwezi huu, kiungo wa Juventus, Nicolo Fagioli kufungiwa miezi saba na FIGC kwa kosa la kwenda kinyume na kanuni za uchezaji kamari.
Tonali na kiungo mwenzake Mtaliano, Nicolo Zaniolo ambaye kwa sasa anaichezea kwa mkopo, Aston Villa, Oktoba 12 mwaka huu waliamriwa kuondoka kwenye kambi ya timu ya taifa ya Italia iliyokuwa Galatasaray kwa kilichoelezwa kuwa walikuwa wakichunguzwa na waendesha mashitaka wa Italia.
Katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Borussia Dortmund iliyopigwa jana Jumatano na Newcastle kulala kwa bao 1-0, Tonali aliingia uwanjani akitokea benchi.
Kimataifa Kamari zamponza kiungo Newcastle, afungiwa miezi 10
Kamari zamponza kiungo Newcastle, afungiwa miezi 10
Read also