Na mwandishi wetu
Wakati vuguvugu la kuondoka kwa Bernard Morrison Simba likiibua hofu, kutoonekana kikosini kwa kiungo wa timu hiyo, Clatous Chama nako kumeibua hofu nyingine ingawa uongozi wa Simba umewatoa wasiwasi mashabiki wake ukiwaeleza kuwa Chama atarejea dimbani kwenye mechi yao dhidi ya Azam.
Hofu hiyo imeibuka kutokana na mazingira ya kuondoka kwa Morrison ambaye hakuonekana baada ya mechi ya Yanga mpaka taarifa ya kupumzishwa kwake katika timu hiyo ilipotolewa jana ambayo pia ilimtakia kila la kheri katika maisha yake ya soka hapo baadaye.
Kama ilivyo kwa Morrison, Chama naye hajaonekana katika kikosi cha timu hiyo baada ya mechi ya Yanga lakini Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Simba, Ahmed Ally ameeleza kuwa Chama bado yupo sana Simba na amekuwa haonekani kutokana na jeraha la goti na pengine anaweza kuonekana kwenye mchezo wa ligi unaofuata dhidi ya Azam.
“Hapana Chama yupo sana, hajaonekana kwa sababu ameumia goti lakini hakuna kingine kama inavyoelezwa, juzi alianza mazoezi na nafikiri kwenye mchezo ujao wa ligi dhidi ya Azam kama atakuwa fiti basi kocha anaweza kumtumia, hili la Morrison haliwezi kuwa kama la Chama, niwaambie wapenzi wa Simba wasiwe na wasiwasi na hilo,” alisema Ally.
Ally pia alibainisha kuwa ishu ya Morrison ilikuwa ni maelewano ya pande mbili baada ga kufuatwa na mchezaji mwenyewe na kueleza kilichopo lakini kuhusu Chama hakuna mawasiliano yoyote yanayofanana na hayo hivyo kila kitu kinakwenda sawa.
Soka Baada ya Morrison, Chama naye aibua maswali
Baada ya Morrison, Chama naye aibua maswali
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
