Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa Azam FC, Youssouph Dabo amesema mshambuliaji wake, Alassane Diao (pichani kushoto) anahitaji muda ili kuwa katika kiwango chake.
Akizungumza Dar es Salaam leo Alhamisi, kocha huyo alisema Diao anahitaji muda kuzoea mazingira lakini pia, anahitaji kupewa nafasi ili kuonesha kile alichonacho.
“Diao anahitaji muda kwa sababu hata wachezaji wenzake hawafahamu uchezaji wake, hawamuelewi vizuri, naamini muda si mrefu watamuelewa na kutupa kile tunakichotarajia kutoka kwake,” alisema.
Mchezaji huyo aliyetokea klabu ya US Goree ya Senegal hajaonesha ubora unaotarajiwa na wengi kama ilivyoelezwa wakati akisajiliwa na Azam huku akiwa amepewa dakika chache uwanjani katika mechi za hivi karibuni za Azam.
Katika mechi mbili za Ligi Kuu NBC, Kombe la Shirikisho Afrika na za Ngao ya Jamii, mchezaji huyo hakupata nafasi ya kuanza kwenye kikosi cha kwanza, aliishia kwenye benchi la timu hiyo.
Soka Kocha Azam amtetea Diao
Kocha Azam amtetea Diao
Read also