Na mwandishi wetu
Kocha Bakari Shime wa timu ya soka ya Taifa ya wasichana chini ya miaka 17, Serengeti Girls anaamini wapinzani wao Cameroon watakuja kucheza kama wapo nyumbani kwa kuwa hawana cha kupoteza.
Kwa kulifahamu hilo, Shime amesema kwamba anawaandaa wachezaji wake kuhakikisha wanapata bao la mapema huku wakizuia vizuri ili kuwapa wakati mgumu wapinzani wao.
Serengeti itajitupa kwenye dimba la Amaan, Zanzibar Jumapili hii kuumana na Cameroon katika mechi ya marudiano ya kuwania kufuzu fainali za Kombe la Dunia ikiwa na faida ya ushindi wa mabao 4-1 katika mechi yake ya awali ambayo Serengeti ilikuwa ugenini.
Katika kuiandaa timu yake kwenye mechi hiyo, Shime amesema kwamba anatambua kuwa wapinzani wao watacheza kwa lengo la kushambulia ili wapate bao jambo ambalo analifanyia kazi kwa kuwaandaa wachezaji wake ili kupata bao la mapema huku wakiwa makini katika kujilinda vizuri ili kuzima ndoto za wapinzani wao.
“Hawa Cameroon hawatakuwa na cha kupoteza, watakuja kucheza mchezo huu kama wako nyumbani, hawatajilinda badala yake watakuwa wakishambulia kwa lengo la kupata bao,” alisema Shime na kuongeza kuwa hata kama yeye angekuwa kocha wa Cameroon hiyo ndiyo ingekuwa mbinu yake.
Shime pia alitahadharisha kwamba pamoja na ukweli huo lakini alitaka watu watambue kwamba mchezo bado upo hai kwani mbinu zitaendelea kuwapo na ufundi kuanzia mwanzo kulitambua hilo lakini bali watashambulia kupata bao hata ningekuwa mimi ndo kocha wao ningefanya hivyo,” alisema Shime
“Tumewaweka wasichana katika kutambua hilo na kuwaeleza ni namna gani sisi tunaweza kufunga bao la mapema litakalozima zima ndoto zao na kujilinda vizuri wasipate bao,” aliongeza.
Shime hata hivyo alitahadharisha kuwa mechi hiyo haitokuwa rahisi na anapenda watu watambue hali halisi kuwa mchezo bado upo hai kwa maana ya mbinu na ufundi.
Serengeti Girls inahitaji ushindi wowote ili kufuzu na ikifanikiwa kufuzu itakuwa timu ya kwanza ya soka kufuzu kwa Tanzania kushiriki mashindano ya dunia ukiacha ile ya soka la watu wenye ulemavu ya Tembo Warriors.
Katika fainali za dunia kwa wanawake zitakazofanyika nchini India kati ya Oktoba 11 hadi 30, Afrika itawakilishwa na timu tatu na hadi sasa timu zenye nafasi kubwa ya kufuzu ni Nigeria, Ghana na Tanzania, Ghana wao wamebakisha mechi na Morocco wakati Nigeria imebakisha mechi na Ethiopia.
Michuano hiyo awali ilipangwa kufanyika mwaka 2021 lakini ilishindikana kutokana na janga la ugonjwa wa corona.
Soka Shime hawachukulii poa Cameroon
Shime hawachukulii poa Cameroon
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
