Na mwandishi wetu
Kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Soka Afrika (Caf) limemfungia mechi nane kocha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, Adel Amrouche na tayari Hemed Morocco ameteuliwa kukaimu nafasi yake.
Taarifa iliyotolewa jioni ya leo Ijumaa na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imeeleza kuwa Caf imefikia hatua hiyo baada ya malalamiko yaliyowasilishwa na Shirikisho la Soka la Morocco (RMFF) dhidi ya Amrouche.
RMFF ilimlalamikia kocha huyo kwa kauli zake kuwa Morocco ina ushawishi ndani ya Caf kwa kuamua wacheze muda gani na kuamua waamuzi wa mechi zao.
“Katika hatua nyingine, Kamati ya Utendaji ya TFF imemsimamisha kocha Adel Amrouche. Kutokana na uamuzi huo, imemteua Hemed Morocco kuwa kaimu kocha na atasaidiwa na Juma Mgunda,” ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Amrouche raia wa Algeria, alitoa kauli hiyo siku moja kabla ya mchezo wa kwanza wa Afcon wa Stars dhidi ya Morocco ambao Stars walilala kwa mabao 3-0.
Mara baada ya Amrouche kutoa kauli hiyo, Rais wa TFF, Wallace Karia alieleza kuwa kauli hiyo ni ya kocha Amrouche na si msimamo wa TFF.
Karia pia alisema kwamba TFF ina mahusiano mazuri na Caf na kufafanua suala la muda wa mechi kuchezwa si la Caf pekee bali hata wadhamini wanahusika nalo na kutolea mifano ya baadhi ya mechi za Ligi Kuu NBC.
Kimataifa Caf yamfungia Amrouche mechi 4, TFF yamuongezea adhabu
Caf yamfungia Amrouche mechi 4, TFF yamuongezea adhabu
Read also