Na mwandishi wetu
Klabu ya Yanga imeeleza kuachana na winga Jesus Moloko (pichani) raia wa DR Congo huku watani zao, Simba SC wakiweka wazi usajili wa straika wao mpya, Pa Omar Jobe kutoka Gambia.
Moloko anapishana na Jobe katika viunga vya Kariakoo, Dar es Salaam zilizopo maskani ya timu hizo baada ya kudumu Jangwani kwa misimu miwili na nusu.
Yanga imeweka wazi hilo leo Jumatatu kwenye mitandao yake ikieleza kuachana na mchezaji huyo wa zamani wa AS Vita ya DR Congo baada ya makubaliano ya pande zote mbili.
Simba nao wameeleza kuinasa saini ya Pa Jobe raia wa Gambia, kuongeza nguvu katika kikosi chao kama ambavyo hivi karibuni kocha wao, Abdelhak Benchikha alivyonukuliwa akieleza kuhitaji mshambuliaji mpya katika kikosi hicho.
Jobe amejiunga na Simba baada ya kumalizana na FC Zhenis ya Kazakhstan na tayari ametuma ujumbe akieleza: “Habari mashabiki wa Simba, mimi ni Pa One, natumai tutaonana hivi karibuni na kufunga mabao mengi, twenzetu.”
Soka Moloko out Yanga, Simba yashusha straika
Moloko out Yanga, Simba yashusha straika
Read also