Manchester, England
Katika mkakati wa kuimarisha safu ya kiungo, Manchester United inadaiwa kuanza mipango ya kumsajili kiungo Mbrazil wa Real Madrid, Casemiro kwa ada inayotajwa kufikia Euro 20 milioni au zaidi.
Mpango huo ukikamilika, Casemiro mwenye umri wa miaka 30 atakuwa ni mchezaji anayelipwa pesa ndefu katika klabu hiyo inayotumiwa Uwanja wa Old Trafford ambayo mambo yake bado hayajaanza kuwa mazuri kwenye Ligi Kuu England msimu huu ikiwa tayari imepoteza mechi mbili za mwanzo.
Casemiro amekuwa kwenye kikosi cha Real Madrid tangu mwaka 2013 akibeba mataji matatu ya La Liga na matano ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, anatakiwa na Man Utd ambayo ilikwama katika mipango yake ya awali ya kumsajili kiungo wa Juventus, Adrienku Rabiot kwa kilichodaiwa kuwa ni mahitaji makubwa ya mchezaji huyo.
Casemiro anaaminika kuwa katika mipango ya kocha Erik ten Hag kuimarisha safu ya kiungo ya Man Utd na imani ya kumpata inatoka na ukweli kwamba nafasi ya mchezaji huyo ndani ya kikosi cha Real Madrid inaweza kuwa njia panda baada ya kusajiliwa kwa Aurelien Tchouameni.
Casemiro ambaye yumo kwenye orodha ya wachezaji 30 wanaowania Ballon D’Or, anatajwa kuwa kati ya viongo wakabaji bora duniani, katika msimu wa 2014/15 aliuzwa kwa mkopo katika klabu ya Porto ya Ureno lakini alirudi Real Madrid msimu uliofuata na hadi sasa ameichezea timu hiyo jumla ya mechi 222 na kufunga mabao 24.
Kimataifa Casemiro wa Madrid atakiwa Old Trafford
Casemiro wa Madrid atakiwa Old Trafford
Read also