Barcelona imeilaza Cadiz mabao 4-0 katika mechi ya La Liga wikiendi hii, ushindi ambao kwa kiasi kikubwa umebebwa na mabadiliko yaliyofanywa na kocha wa timu hiyo, Xavi Harnandez baada ya mambo kuwa magumu kipindi cha kwanza.
Mabao yote manne ya Barcelona yalipatikana kipindi cha pili baada ya Xavi kuipangua timu yake ingawa kocha huyo hakuwa tayari kukubali kwamba ushindi huo mnono umetokana na mabadiliko aliyoyafanya.
Barca iliyokuwa ugenini inaaminika kocha wake aliamua kuwapumzisha baadhi ya mastaa wake ili wawe fiti katika mechi ya Ligi ya Mabingwa Ulaya dhidi ya Bayern Munich.
Gerard Pique na Ronald Araujo walianza katika ulinzi wa kati huku Hector Bellerin akianza katika nafasi ya beki wa kulia na Alejandro Balde akaendelea na beki ya kushoto.
Baadaye Frenkie de Jong akaingia kuchukua nafasi ya Pedri katika safu ya kiungo na kuungana na Sergio Busquets na Gavi. Katika safu ya ushambuliaji walianza Ferran Torres, Memphis Depay na Raphinha, timu hiyo kidogo ilipata shida kuisumbua Cadiz. Kasi ya mchezo ilianza kuonekana kwa Barca baada ya kuingia kwa Pedri, Ousmane Dembele na Robert Lewandowski.
Xavi alimuingiza Lewandowski katika dakika ya 57 wakati Barca ikiwa mbele kwa bao moja na baada ya hapo ikawa kama Lewandowski kaingia na silaha ya maangamizi, kasi ya Barca ikaongezeka na hadi filimbi ya kumaliza mchezo inapulizwa Barca wakatoka na mabao 4-0.
Mabao ya Barcelona yalifungwa na de Jong dakika 10 baada ya mapumziko, Lewandowski dakika ya 65, Fati Vieira dakika ya 86 na Dembélé katika dakika za nyongeza.
Real Madrid nao wikiendi imekuwa nzuri kwao baada ya kuichapa Real Mallorca mabao 4-1. Mallorca waliokuwa ugenini walikuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Vedat Muriqi lakini Federico Valverde kabla Vinicius hajaongeza bao la pili wakati mabao mengine ya washindi yalifungwa na Rodrygo na Antonio Rudiger.
Matokeo ya La Liga wikiendi hii ni kama ifuatavyo
Real Madrid 4-1 Mallorca
Elche 1- 4 Ath Bilbao
Getafe 2-1 Real Sociedad
Real Betis 1-0 Villarreal
Rayo Vallecano 2-1 Valencia
Espanyol 2-3 Sevilla
Cadiz 0-4 Barcelona
Atlético Madrid 4-1 Celta Vigo
Girona 2-1 Real Valladolid
Kimataifa Xavi aipangua Barca, yashinda 4-0
Xavi aipangua Barca, yashinda 4-0
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
