London, England
Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amemshutumu msimamizi wa VAR, David Coote kwa alichodai kuwa ni timu yake imenyimwa penalti katika mechi ya Ligi Kuu England (EPL) dhidi ya Arsenal iliyoisha kwa sare ya bao 1-1.
Klopp ambaye timu yake kwa sasa inapambana vikali na Arsenal kuwania kushika usukani EPL, alisema walitakiwa kupewa penalti baada ya Martin Odegaard kuunawa mpira katika mechi hiyo iliyopigwa jana Jumamosi.
Sare hiyo iliyopatikana kwa mabao ya Gabriel mapema dakika ya nne na kabla ya Mohamed Salah kuisawazishia Liverpool, yanaifanya Arsenal kula Krismasi ikiwa kileleni mwa msimamo wa EPL ikiidizi Liverpool kwa pointi moja.
Akizungumzia tukio hilo la dakika ya 19, Klopp alisema kwamba Odegaard alionekana akitumia mkono kuzuia mpira uliopigwa na Salah kwa kuunawa ndani ya eneo la 18.
Mwamuzi, Chris Kavanagh aliruhusu mpira kuendelea na hakukuwa na tukio la kusimamisha mpira ili kuangalia VAR huku Coote akidai kwamba Odegaard aliunawa mpira wakati akianguka.
“Ndio nimeona, nina hakika kabisa kwamba kuna mtu atakuja kunielezea ni kwa nini haikuwa mtu kuunawa mpira lakini sijui ni kwa namna ipi,” alisema Klopp.
“Siwezi kusema kwamba mwamuzi anaweza kuona kwa sababu sijui alikuwa wapi wakati wa tukio lile, lakini inawezekanaje mtu aliyekuwa ofisini aone kwa namna ile na asije na hitimisho labda kwa mwamuzi kuangalia kwa mara nyingine,” alisema Klopp.
Alipoulizwa kuhusu tukio hilo, kocha wa Arsenal, Mikel Arteta alisema kwamba kulikuwa na maamuzi makubwa mawili ambayo hakuyaangalia kwa mara nyingine, matukio ambayo aliulizwa kabla lakini yote hakuyaangalia kwa mara nyingine.
Matokeo ya mechi za EPL jana Jumamosi…
West Ham 2-0 Man Utd
Fulham 0-2 Burnley
Luton 1-0 Newcastle
Nottm Forest 2-3 Bournemouth
Tottenham 2-1 Everton
Liverpool 1-1 Arsenal
