Na mwandishi wetu
Mshambuliaji wa Tanzania, Simon Msuva ameachana wa waajiri wake, JS Kabylie ya Algeria kwa makubaliano maalum ikiwa ni miezi minne tangu ajiunge nao Agosti 28 mwaka huu kwenye dirisha kubwa la usajili.
Msuva alijiunga na Kabylie kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Al Qadisiah ya Falme za Kiarabu ambako alionyesha kiwango cha hali ya juu na kuwavutia wabishi hao wa Algeria.
Katika kipindi cha miezi minne aliyodumu katika kikosi cha Kabylie, Msuva alicheza michezo sita ya ligi kuu akiwa hajafunga bao wala kutoa pasi ya mwisho katika dakika 245 alizohudumu uwanjani.
Msuva mwenye umri wa miaka 30 hivi sasa kwa mujibu wa mtandao wa Transfer Market ana thamani ya Dola 500,000 ambazo ni sawa na Sh bilioni 1.2.
Hii inakuwa timu ya saba Msuva kuichezea tangu alipoanza kucheza soka la kulipwa mwaka 2011 akiwa na Azam FC ambapo amepita pia Moro United, Yanga, Difaa El Jadida, Wydad AC pamoja na Al-Qadsiah.
Kimataifa Msuva, JS Kabylie waachana
Msuva, JS Kabylie waachana
Read also