Na mwandishi wetu
Waziri wa Vijana, Michezo na Sanaa wa Kenya, Ababu Namwamba (pichani) ametuma salamu za kuitakia heri timu ya taifa ya Tanzania, ‘Taifa Stars’ kwenye michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika (Afcon 2023) iliyoanza jana Jumamosi nchini Ivory Coast.
Akizungumza na vyombo vya habari vya nchini Kenya, Namwamba alisema Afrika Mashariki inawakilishwa na Tanzania katika mashindano ya hayo hivyo wanahitaji maombi maalumu.
“Kwa niaba ya timu ya pamoja ya Afrika Mashariki tunawakia ndugu zetu Watanzania kila la heri kwenye michuano ya Afcon, Taifa Stars wanahitaji maombi maalumu kama wawakilishi wetu Ivory Coast,” alisema.
Taifa Stars ndio timu pekee ya Ukanda wa Afrika Mashariki inayoshiriki mashindano hayo ya 34 yaliyoanza jana yakishirikisha mataifa 24 ambapo Stars ipo Kundi F na timu za Morocco, DR Congo na Zambia.
Jumatano ijayo Tanzania itacheza na Morocco, Januari 21 dhidi ya Zambia na itamaliza mechi zake za makundi kwa kuikabili DR Congo, Januari 24, mwaka huu.
Kiungo wa Yanga raia wa Uganda, Khalid Aucho pia alieleza anaisapoti Tanzania katika michuano hiyo baada ya kuweka picha katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram akiwa na uzi wa Stars.
Kimataifa Waziri Kenya aitakia mafanikio Stars
Waziri Kenya aitakia mafanikio Stars
Read also