Na mwandishi wetu
Dodoma Jiji imewataka mashabiki wake kutokata tamaa licha ya timu hiyo kuwa kwenye hali mbaya katika msimamo wa ligi msimu huu kwa kuwa wanajua kinachowaangusha na wameanza kukifanyia kazi.
Timu hiyo ambayo ilianza kukosa matokeo tangu kwenye mechi za mwanzoni mwa ligi kwa sasa inashika nafasi ya 12 kwa pointi 24, tofauti ya pointi tano dhidi ya Ruvu Shooting inayoburuza mkia.
Kocha Msaidizi wa Dodoma, Kassim Liogope alisema: “Ni kweli hatupo kwenye nafasi nzuri baada ya kupoteza michezo miwili iliyopita, lengo letu lilikuwa tushinde hizo mechi lakini sasa mapungufu tumeyaona, haswa ni kushindwa kutumia nafasi za kufunga lakini tayari tumeanza kuyafanyia kazi.
“Mashabiki na wapenzi hawapaswi kukataa tamaa katika hali hii kwani tunafahamu bado michezo michache lakini tunapambana na tunafanya juhudi za kutosha kuhakikisha tunamaliza ligi tukiwa salama,” alisema Liogope.
Dodoma ambayo imepata ushindi wa mechi moja katika mechi zake tano zilizopita, imebakiza mechi dhidi ya Polisi Tanzania, Coastal Union, KMC, Yanga, Namungo na Ruvu Shooting.
Timu hiyo inapaswa kupambana isishuke zaidi ya nafasi iliyopo sasa kwani ikimaliza nafasi ya 13 na 14 italazimika kucheza mechi za mtoano kuwania kusalia Ligi Kuu msimu ujao na ikimaliza chini ya hapo itashuka daraja moja kwa moja.
Soka Dom Jiji hakuna kukata tamaa
Dom Jiji hakuna kukata tamaa
Read also