Na mwandishi wetu
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan na Rais wa Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi wamenunua tiketi zote za mechi kati ya timu ya taifa ya wanawake ya Tanzania ‘Tanzanite Queens na Cameroon.
Timu hizo mbili zitaumana kesho Jumapili, Mei 10, 2026 kwenye Uwanja wa New Amaan, Zanzibar na kwa hatua ya viongozi hao, mashabiki watapata fursa ya kuingia uwanjani bure kuzishuhudia timu hizo zikichuana.
Kwa mujibu wa taarifa ya TFF, mechi hiyo itachezwa kuanzia saa 10 alasiri na timu hizo zitakuwa zinasaka tiketi ya fainali za Kombe la Dunia kwa wanawake zitakazochezwa Septemba mwaka huu nchini Poland.
Lengo la viongozi hao kuamua kununua tiketi zote za mechi hiyo ni kuongeza hamasa kwa kuruhusu mashabiki wengi zaidi kushuhudia mechi hiyo muhimu kwa Tanzanite Queens.
Kwa mujibu wa TFF hii si mara ya kwanza kwa viongozi hao kununua tiketi kwa lengo la kuruhusu mashabiki kuingia uwanjani bure.
Tanzania Queens ina kazi kubwa ya kufanya ili kusonga mbele baada ya kuchapwa mabao 3-1 katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo iliyochezwa mjini Yaounde, Cameroon.
Kimataifa Mechi Tanzanite Queens, Cameroon haina kiingilio
Mechi Tanzanite Queens, Cameroon haina kiingilio
Read also
