London, England
Bao pekee la Harry Kane lililoiwezesha Tottenham Hotspur kupata ushindi wa 1-0 dhidi ya Fulham limemfanya mshambuliaji huyo kuweka rekodi ya kuwa mfungaji wa timu hiyo mwenye mabao mengi akimfikia Jimmy Greaves, kila mmoja akiwa na mabao 266.
Greaves ambaye ni marehemu kwa kipindi kirefu alikuwa akishikilia rekodi ya kuwa na mabao mengi katika timu hiyo lakini hatimaye jana Jumatatu Kane alifunga bao lililomfanya kuingia katika kundi moja na Greaves wote wakiwa sawa kwa kila mmoja kufunga mabao 266.
Tofauti ya Kane na Greaves kwa sasa ni mechi walizocheza hadi kufikia idadi hiyo ya mabao, Greaves aliifikia rekodi hiyo katika mechi 379 wakati Kane ameifikia katika mechi 415.
Kwa upande mwingine, Kane ambaye pia ni nahodha wa England, bado ana nafasi ya kuiendeleza rekodi hiyo wakati wowote msimu huu na hatimaye kuwa mfungaji mwenye mabao mengi katika historia ya klabu hiyo.
Kane pia atakuwa na kazi mbili, moja ni kuongeza mabao ili kuwa kinara wa mabao wa wakati wote wa Spurs lakini pia anahitaji kufunga bao moja la ligi ili kufikisha mabao 200 na kuingia katika rekodi inayoshikwa na mastraika wa zamani wa England, Wayne Rooney na Alan Shearer.
Ushindi huo mbali na kumfanya Kane aingie katika orodha ya mchezaji mwenye mabao mengi katika historia ya klabu hiyo pia umefufua upya matumaini ya Spurs katika mbio za kusaka nafasi ya nne bora.
Kwa sasa Spurs inashika nafasi ya tano ikiwa na pointi 36, imezidiwa na timu za Newcastle ambayo inashika nafasi ya tatu na Man United inayoshika nafasi ya nne kwa tofauti ya pointi tatu.
Kimataifa Kane aweka rekodi Spurs
Kane aweka rekodi Spurs
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
