Salonika, Ugiriki
Nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Mbwana Samatta amejiunga na klabu ya PAOK FC inayoshiriki Super Ligi nchini Ugiriki akitokea Fenerbahçe ya Uturuki.
Samatta aliyewahi kutamba na timu za Afrcan Lyon na Simba za Tanzania, alijiunga na TP Mazembe ya DR Congo mwaka 2010 na kudumu kwa miaka mitano akiwa mmoja wa wachezaji tegemeo wa timu hiyo.
Akiwa TP Mazembe ndipo nyota yake ilipoanza kung’ara kimataifa hadi kutwaa tuzo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) ya mwanasoka bora anayecheza soka Afrika mwaka 2015.
Ni katika kipindi hicho hicho ndipo Samatta pia aliibuka mfungaji bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika akiiwezesha Mazembe kubeba taji la ligi hiyo na kushiriki michuano ya klabu ya dunia.
Mwaka 2016, Mazembe walimuuza katika klabu ya KRC Genk ya Ubelgiji aliyoiwezesha kufuzu michuano ya Europa Ligi kabla ya kuibukia katika Ligi Kuu England mwaka 2020 alipojiunga na Aston Villa ingawa Septemba mwaka huo huo aliuzwa kwa mkopo katika klabu ya Fenerbahce.
Nyota ya Samatta hata hivyo haikung’ara sana na klabu hiyo ya Uturuki ambayo ilimpeleka kwa mkopo katika klabu ya Royal Antwerp ya Ubelgiji kabla ya kurejea Genk mwaka 2022.
Baada ya kujiunga na POAK ambayo ni moja ya timu tano bora nchini Ugiriki kwenye Super Ligi, Samatta sasa ataonekana akiiwakilisha timu hiyo hiyo na michuano mipya ya Europa Conference Ligi.
Michuano ya Europa Conference Ligi ni ya tatu kwa ukubwa katika ligi za klabu za barani Ulaya ikiwa imetanguliwa na Ligi ya Mabingwa na Europa Ligi.
Kimataifa Samatta ahamia PAOK FC ya Ugiriki
Samatta ahamia PAOK FC ya Ugiriki
Read also