Na mwandishi wetu
Burudani ya soka ya Ligi Kuu NBC itasimama kwa kipindi cha miezi miwili kuanzia Desemba 29 mwaka jana na kurejea Machi Mosi, 2025 kutokana na matukio kadhaa ya kimichezo.
Taarifa ya idara ya mawasiliano ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) iliyopatikana Desemba 31 iliyataja matukio mawili yanayosababisha kusimamishwa kwa ligi hiyo.
Matukio hayo ni michuano ya Kombe la Mapinduzi itakayofanyika kisiwani Pemba pamoja na fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa ndani (Chan) ambazo Tanzania ni mmoja wa wenyeji.
TPLB ilifafanua kuwa licha ya changamoto hiyo lakini wamejipanga kuhakikisha msimu wa ligi hiyo wa 2024-25 unafikia tamati kwa mujibu wa kanuni za ligi na kutoathiri kipindi cha mapumziko na maandalizi ya msimu ujao wa 2025-26.
Bodi pia inaamini klabu zitakitumia vyema kipindi hiki cha mapumziko kwa kufanya maboresho na marekebisho katika vikosi vyao ili kuendana na ushindani mkubwa uliopo kwenye ligi hiyo.
Taarifa ya bodi ilimalizia kwa kuitakia kila la kheri timu ya taifa ya Tanzania katika maandalizi ya Chan pamoja na kuwatakia heri ya mwaka mpya wa 2025 wadau wote wa mpira wa miguu nchini.
Soka Miezi miwili bila Ligi Kuu NBC
Miezi miwili bila Ligi Kuu NBC
Read also
