Doha, Qatar
Winga wa England, Raheem Sterling kesho Ijumaa anatarajia kurejea Qatar kwenye kikosi cha England tayari kwa ajili ya mechi ya Jumamosi ya robo fainali ya Kombe la Dunia dhidi ya Ufaransa.
Sterling mwenye miaka 28 ambaye pia ni mchezaji wa Chelsea, Jumapili iliyopita alilazimika kurudi England baada ya majambazi kuvamia nyumbani kwake Surrey wakati familia yake yenye watoto watatu wadogo wakiwa ndani na yeye akiwa Qatar na kikosi cha England.
Kwa kuondoka huko Sterling alikosa mechi ya England ya hatua ya mtoano dhidi ya Senegal, mechi ambayo hata hivyo England ilishinda kwa mabao 3-0 na kufuzu kucheza robo fainali na sasa inasubiri kuumana na Ufaransa keshokutwa, Jumamosi.
Sterling ambaye pia aliwahi kuzichezea Man City na Liverpool, alishtushwa na tukio la familia yake kuvamiwa na kuanza kuwafikiria watoto wake wadogo hivyo akaamua kurudi England ili kuifariji familia hiyo.
Taarifa ya Polisi wa Surrey ilieleza kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi wa taarifa ya uvamizi baada ya mmiliki wa nyumba kurudi kwake na kukuta vito vya thamani vimeibiwa lakini hakuna uhalifu na uharibifu wowote uliofanyika.
Hadi sasa hakuna mtuhumiwa yeyote aliyekamatwa akihusishwa na uhalifu huo ingawa taarifa ya polisi ilikataa kulihusisha tukio hilo na tukio lingine la uhalifu linalofanana na hilo lililotaka kufanyika katika eneo hilo hilo.
Kimataifa Sterling arudi kikosini England
Sterling arudi kikosini England
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
