Munich, Ujerumani
Bayern Munich imeendelea kujipa matumaini makubwa ya kumsajili mshambuliaji Harry Kane wa Tottenham Hotspur, licha ya PSG nayo kudaiwa kujiimarisha zaidi katika kuhakikisha inampata mshambuliaji huyo.
Ofisa mtendaji mkuu wa Bayern, Jan-Christian Dreesen na mkurugenzi wa ufundi, Marco Neppe inadaiwa hawajaungana na timu hiyo nchini Japan kwa ziara ya maandalizi ya msimu mpya ili wapate muda wa kushughulikia usajili wa Kane.
Vigogo hao wawili inadaiwa wanajiandaa kuwasilisha ofa ya tatu ambayo inatajwa kufikia Pauni 100 milioni ili kumnasa mshambuliaji huyo ambaye Spurs wanataka kumtumia kutunisha mfuko wao.
Matumaini ya Bayern yamezidi kuwa makubwa hivi karibuni baada ya Spurs kutaka auzwe huku Kane mwenyewe akidai kwamba angependa zaidi kujiunga na Bayern na si PSG.
Wakati Bayern ikiwa na matumaini, PSG nayo inadaiwa kujipanga kumwaga fedha za kuishawishi Spurs ikubali kuwauzia mshambuliaji huyo ambaye pia anaichezea timu ya Taifa ya England.
Tayari PSG imetangaza kumuuza mshambuliaji wake, Kylian Mbappe ambaye anatakiwa na klabu za Real Madrid na Al Hilal ya Saudi Arabia inayojiandaa kuweka rekodi ya dunia kwa kumsajili kwa Pauni 259 milioni.
PSG inaamini mauzo ya Mbappe yatawapa jeuri ya fedha za kuifanya Spurs ishawishike kumuuza mchezaji katika klabu hiyo ya nchini Ufaransa badala ya Bayern.
Ukiacha Real Madrid na Al Hilal, klabu nyingine zinazodaiwa kumtaka Mbappe ni Chelsea, Tottenham, Inter Milan, Man United na Barcelona.
Kimataifa Bayern matumaini kibao kwa Kane
Bayern matumaini kibao kwa Kane
Read also