London, England
Nyota wa Manchester City, Benjamin Mendy amefutiwa shitaka la kumbaka msichana wa miaka 19 katika mahakama ya Chester Crown baada ya kuonekana hana hatia.
Mendy na mtuhumiwa mwenzake Louis Saha Matturie, pia wamefutiwa mashitaka mawili ya kubaka na udhalilishaji wa kijinsia, vitendo walivyokuwa wakituhumiwa kumfanyia msichana huyo baada ya waendesha mashitaka kutokuwa tayari kutoa ushahidi zaidi dhidi ya watuhumiwa wa makosa hayo.
Sambamba na hatua hiyo Jaji Stephen Everett alitaka uchunguzi ufanywe ili ijulikane ni kwanini watuhumiwa wamekuwa wakiongezewa mashitaka ya aina hiyo hiyo wanayokabiliwa nayo.
Shtaka ambalo Mendy amefutiwa katika mahakama hiyo juzi Jumanne linahusisha tukio ambalo mwanasoka huyo anadaiwa kulifanya Julai 24 mwaka jana akiwa nyumbani kwake.
Mendy hata hivyo pamoja na kufutiwa mashitaka hayo bado anakabiliwa na mashitaka mengine saba ya kubaka, moja la kuwa na damira ya kubaka na moja la udhalilishaji wa kijinsia dhidi ya wasichana sita ambapo waendesha mashitaka walidai kwamba Mendy alikuwa na tabia ya kuwarubuni wasichana na kuwatumia katika namna ya kuwadhalilisha ambapo rafiki yake Matturi naye anadaiwa kuwa ndiye aliyekuwa akifanya kazi ya kumtafutia Mendy wasichana hao.
Mendy ambaye baada ya tuhuma hizo alisimamishwa na klabu yake ya Man City yeye na Matturie, wamekana tuhuma hizo na kudai kwamba wasichana wote wanahusishwa katika masuala ya ngono walifanya hivyo kwa makubaliano na hivyo hakuna udhalilishaji wowote uliofanywa.
Kimataifa Mendy afutiwa shtaka la ubakaji
Mendy afutiwa shtaka la ubakaji
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
