Manchester, England
Polisi wa Manchester wamemuonya mshambuliaji wa Manchester United, Cristiano Ronaldo baada ya kudaiwa kuvunja simu ya shabiki wa soka siku ambayo timu yake ilishindwa kutamba mbele ya Everton katika mechi iliyopigwa Aprili mwaka huu.
Baada ya Man Utd kulala kwa bao 1-0 kwenye dimba la Goodison Park katika mechi ya msimu uliopita, picha za vyanzo mbalimbali vya habari zilimuonyesha Ronaldo akiiangusha chini simu ya shabiki wakati akitoka uwanjani kuelekea kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.
Ronaldo hata hivyo baadaye aliomba radhi kwa tukio hilo na polisi wametoa taarifa yao Jumatano hii kuhusu kilichojiri katika tukio hilo.
“Tunaweza kuthibitisha kwamba mtu mwenye umri wa miaka 37 kwa hiari yake alifika na kuhojiwa akihusishwa na tukio kushambulia na uharibifu,” ilieleza taarifa hiyo.
“Tuhuma hizo zinahusisha tukio lililojitokeza katika mechi kati ya Everton na Manchester United kwenye Uwanja wa Goodison Park, siku ya Jumamosi, Aprili 9, suala hilo limeshughulikiwa katika mazingira ya tahadhari na kufikia hitimisho.”
Kimataifa Polisi wamuonya Ronaldo
Polisi wamuonya Ronaldo
Read also