London, England
Kinda wa Arsenal, Bukayo Saka inadaiwa anasakwa na klabu za Man City na Liverpool ambazo zipo tayari kuvunja mkataba wa mchezaji huyo katika klabu ya Arsenal.
Saka ambaye ndio kwanza ana miaka 20, ni mmoja wa wachezaji wenye umri mdogo wanaotabiriwa mambo makubwa hapo baadaye, ana mkataba na Arsenal ambao unafikia ukomo mwaka 2024 na kinachoonekana ni kama vile hajawa tayari kuuongeza mkataba na klabu hiyo.
Nyota huyo wa England tayari ameonyesha dalili njema akiwa na Arsenal kwa kufunga mabao 12 na kutoa asisti saba katika mechi 43 alizoichezea timu hiyo jambo ambalo linazifanya klabu hizo kuamini kwamba anaweza kuwa msaada kwao hasa ikizingatiwa umri wake mdogo.
Kwa mujibu wa gazeti la Daily Mail, City ambao ni mabingwa wa Ligi Kuu England wanafuatilia kwa karibu masuala ya mkataba wa mchezaji huyo na wako makini katika kuhakikisha wanatia neno ili kumtoa mchezaji huyo Arsenal.
Katika mbio hizo inadaiwa kwamba wapinzani wakuu wa City katika Ligi Kuu England, Liverpool nao hawapo nyuma, wanaangalia nini cha kufanya ili kumpata kinda huyo ambaye anaaminika atakuwa hazina nzuri sasa na baadaye.
Wakati yote hayo yakiendelea, Arsenal nao wanauangalia mpango huo kwa mambo mawili, kumbakisha Saka ili aendelee na mkataba wake au kuhakikisha wanavuna pesa ndefu kwa timu yoyote itakayokuwa tayari kuvunja mkataba wa mchezaji huyo klabuni hapo.
Soka Saka azigombanisha Man City, Liverpool
Saka azigombanisha Man City, Liverpool
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
