Na mwandishi wetu
Kocha Mkuu wa KMC, Thierry Hitimana amefafanua kuwa anatarajia mchezo mgumu kutoka kwa Coastal Union leo, hivyo amekiandaa kikosi chake kucheza kwa tahadhari kuhakikisha wanapata pointi tatu muhimu.
Huo ni mchezo wa kwanza wa KMC wa mzunguko wa pili wa lala salama wa Ligi Kuu ya NBC ambapo Hitimana anahitaji matokeo ili aanze vizuri mzunguko huo tofauti na mzunguko uliopita.
“Tunashukuru Mungu tumemaliza maandalizi salama, tulikuwa na tatizo la majeruhi na ndiyo maana tulishuka kidogo kiuwezo lakini sasa angalau wamepona baadhi na wamebaki wachache na tunajua mechi ni ngumu kutokana na matokeo ya Coastal yaliyopita na kikosi walichonacho.
“Japo mechi ni ngumu kama ilivyo ligi ya msimu huu lakini huu ni ukurasa mwingine, ni mzunguko mwingine inabidi tuanze vizuri na ukiangalia hatujapishana sana na Coastal kwenye msimamo hivyo lazima tuwe makini katika kutafuta pointi maana hata wao wanaliona hilo,” alisema Hitimana.
KMC itashuka kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam ikiwa nafasi ya 10 na pointi 16 wakati Coastal ikiwa nafasi ya 12 na pointi 15.
LigiKuu Hitimana awaza pointi tatu kwa Coastal
Hitimana awaza pointi tatu kwa Coastal
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
