Na mwandishi wetu
Simba imeendelea kujiimarisha katika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu NBC kwa kuichapa Namungo FC mabao 3-1 katika mechi ilyochezwa Jumapili, Aptili 19, 2026 kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa, Lindi.
Kwa ushindi huo, Simba sasa imefikisha point 42 katika mechi 19 ikiwa imetanguliwa na Yanga inayoshika usukani ikiwa na pointi 47 katika mechi 19 kama ilivyo Simba.
Mashabiki wa Simba walianza kushangilia bao la kwanza kwa timu yao katika dakika ya 12 mfungaji akiwa ni Libasse Gueye akimalizia pasi ya Anthony Mligo.
Simba walipambana na kuongeza bao la pili dakika 12 baadaye, bao lililofungwa na Anicet Oura akiitumia vizuri pasi ya Yusuph Kagoma.
Namungo walipambana na kufanikiwa kuzichana nyavu za Simba katika dakika ya 33 kwa bao la Heritier Makambo alilofunga kwa mkwaju wa penalti iliyotolewa baada ya Kagoma kuunawa mpira katika eneo la hatari.
Simba hawakuridhika na mabao hayo mawili na katika dakika ya 74 walifunga bao la tatu mfungaji akiwa ni Ellie Mpanzu, bao lililofuta matumaini ya Namungo kupata bao la kusawazisha.
Kimataifa Simba yaicharaza Namungo 3-1
Simba yaicharaza Namungo 3-1
Related posts
Read also
