Manchester, England
Nahodha wa zamani wa Manchester United, Wayne Rooney inaonekana amempania Cristiano Ronaldo baada ya awali kushauri mchezaji huyo aachwe aondoke, sasa anamtaka kocha wa timu hiyo, Erik ten kumsugulisha benchi katika mechi dhidi ya Liverpool Jumatatu hii.
Rooney ambaye amewahi kucheza na Ronaldo katika timu hiyo, amemtaka Ten Hag pia kumuweka benchi Marcus Rashford katika mechi hiyo..
Wachezaji hao wawili walicheza katika mechi mbili za mwanzo za Man United dhidi ya Brighton na Brentford, mechi ambazo Man Utd ilishindwa kutamba huku Ronaldo akidaiwa kushikilia msimamo wa kutaka kuihama timu hiyo wakati Rashford hajaifungia timu hiyo bao lolote tangu Januari mwaka huu.
Msimu uliopita ulikuwa majanga kwa Man United katika mechi zake na Liverpool ilipolala kwa mabao 5-0 na 4-0 na sasa Rooney, anamtaka Ten Hag kuwaweka benchi wachezaji hao ili kubaki na wachezaji watakaoendana na kiwango cha kasi ya wachezaji wa Liverpool.
“Mimi nisingempanga Cristiano Ronaldo na pia nisingempanga Marcus Rashford katika mechi na Liverpool,” alisema Rooney kupitia Jarida la Sunday Times.
“Kama ningekuwa katika nafasi aliyonayo Ten Hag hofu pekee ambayo ningekuwa nayo ni kuwa na nguvu uwanjani, na kwa Man Utd kushindwa kusajili mchezaji namba 9 maana yake ni kwamba walimtegemea Ronaldo katika mechi dhidi ya Brentford ingawa hakufanya mazoezi kwa muda mrefu na timu, alionekana kama anayehitaji muda wa kuwa fiti kwa ajili ya mechi,” alisema Rooney.
‘Pia ameshaweka wazi kwamba anataka kuondoka, sizijui sababu zake lakini kama nilivyosema huko nyuma, mimi ningemuacha aende, ni mchezaji mzuri na wakati wote anafunga lakini kazi aliyonayo Ten Hag kwa sasa ni kuisuka timu ambayo itapigania mataji katika miaka mitatu au minne ijayo, hiyo maana yake ni kwamba unaijenga timu kwa kuwatumia wachezaji vijana.”
Kimataifa Rooney ataka Ronaldo asugue benchi
Rooney ataka Ronaldo asugue benchi
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
