Na mwandishi wetu
Kikosi cha Singida Fountain Gate kinatarajia kuweka kambi jijini Mwanza kwa ajili ya kujiwinda na michezo miwili ya Ligi Kuu NBC dhidi ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons.
Akizungumza na GreenSports, Ofisa Habari wa Singida FG, Hussein Massanza (pichani) alisema kikosi hicho kimeingia kambini Januari 27 na mwisho kwa wachezaji wote kujiunga na kambi ni Januari 29 huku Januari 30 kocha Thabo Senong akitarajia kuanza program maalumu.
“Tumeamua kuweka kambi maalumu jijini Mwanza kwenye Uwanja wa Gwambina zamani ambao sasa unaitwa Fountain Gate kwa sababu michezo yetu inayofuata itakuwa ugenini Kanda ya Ziwa.
Alifafanua zaidi kuwa kuna mambo kadhaa yalijitokeza na kuleta hofu kwa mashabiki wao kuhusu kuuza wachezaji wao wakahisi huenda wanaweza tukalega lega kwa bahati nzuri walisajili wachezaji kimkakati na wengine wamesalia na timu huku kiufundi akinadi kuwa hawajaathirika na mabadiliko hayo morali ya wachezaji iko juu.
Soka Singida FC kuweka kambi Mwanza
Singida FC kuweka kambi Mwanza
Read also