New York, Marekani.
Jarida maarufu la Forbes limeitaja klabu ya Real Madrid kwa mara ya pili mfululizo kuwa klabu tajiri namba moja duniani kwa mwaka 2022 ikiwa na thamani ya Dola bilioni 6.07 ikifuatiwa na Man United.
Kwa mujibu wa Forbes, jarida lililojijengea umaarufu duniani kote kwa kujikita zaidi katika uchambuzi wa masuala ya uchumi na biashara, Man United imetajwa kuwa na thamani y Dola bilioni 6.
Barcelona ambayo mwaka 2021 iliongoza katika orodha hiyo, safari hii imeangukia katika nafasi ya tatu thamani yake ikifikia Dola bilioni 5.51.
Ripoti ya jarida hilo imefafanua kuwa Real Madrid katika kipindi cha mwaka mmoja imeongezeka thamani yake kwa asilimia 19 wakati Man United kwa asilimia 30 lakini pia hii ni mara ya kwanza kwa thamani ya klabu kufikia Dola bilioni 6.
Klabu za Real Madrid na Man United ndizo pekee ambazo zimekuwa katika tano bora ya orodha hiyo kila mwaka tangu jarida hilo lianze utaratibu wa kutoa ripoti hizo mwaka 2004.
Katika orodha hiyo, timu sita za Ligi Kuu England (EPL) zimo kwenye ‘top ten’ ambapo Arsenal inashika nafasi ya 10 ikitanguliwa na Tottenham iliyo nafasi ya tisa.
Orodha kamili ya top ten za Jarida la Forbes na thamani yake kwenye mabano ni kama ifuatavyo…
- Real Madrid ($6.07bn)
- Manchester United ($6bn)
- Barcelona ($5.51bn)
- Liverpool ($5.29bn)
- Manchester City ($4.99bn)
- Bayern Munich ($4.86bn)
- Paris Saint-Germain ($4.21bn)
- Chelsea ($3.1bn)
- Tottenham Hotspur ($2.8bn)
- Arsenal ($2.26bn)