London, England
Arsenal hatimaye imefanikiwa kushika usukani wa Ligi Kuu England (EPL) kwa mara ya kwanza tangu Desemba mwaka jana baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Brentford ingawa huenda ikakaa kileleni muda usiozidi saa 24.
Ushindi huo wa Jumamosi hii jioni ulitokana na mabao ya Declan Rice dakika ya 19 na Kai Havert dakika ya 86 wakati bao pekee la Brentford lilipatikana dakika ya 45 mfungaji akiwa ni Yoane Wissa,
Matokeo hayo yameifanya Arsenal kufikisha pointi 64 katika mechi 28 ikifuatiwa na Liverpool inayoshika nafasi ya pili ikiwa na pointi 63 na Man City ya tatu yenye pointi 62,
Man City na Liverpool kila moja imecheza mechi 27 na Jumapili hii timu hizo zinaumana katika mechi ngumu ambayo matokeo yake yatakuwa sababu ya kuiengua Arsenal kileleni mwa msimamo huo.
Faraja pekee kwa Arsenal ni timu hizo kutoka sare ambayo itaifanya Liverpool kufikisha pointi 64 kama za Arsenal na hivyo kushindana kwa tofauti ya mabao ya kufunga na kufungwa na Man City watafikisha pointi 63 na kuendelea kuwa nyuma ya Arsenal.
Tofauti na matokeo hayo ushindi wa aina yoyote katika mechi hiyo utaitoa Arsenal kileleni, Liverpool ikishinda itakuwa imefikisha pointi 66 wakati Man City ikishinda itakuwa imefikisha pointi 65.
Matokeo ya mechi za EPL Jumamosi hii…
Man Utd 2-0 Everton
Bournemouth 2-2 Sheff Utd
Crystal Palace 1-1 Luton
Wolves 2-1 Fulham
Arsenal 2-1 Brentford
Kimataifa Arsenal yashika usukani EPL
Arsenal yashika usukani EPL
Read also