Sydney, Australia
Nigeria leo Alhamisi imeipeperusha vyema bendera ya Afrika kwenye fainali za Kombe la Dunia za Wanawake baada ya kuwalaza wenyeji Australia kwa mabao 3-2 na kushika usukani katika Kundi F.
Matokeo hayo yanawaweka Australia katika wakati mgumu kufuzu hatua inayofuata ya timu 16 kwani sasa italazimika kushinda mechi inayofuata dhidi ya Canada ili kuendelea katika hatua hiyo.
Katika mechi hiyo, Australia ndio waliokuwa wa kwanza kupata bao lililofungwa na Emily van Egmond muda mfupi kabla ya timu kwenda mapumziko akiitumia vyema pasi ya Caitlin Foord’s
Nigeria hata hivyo iliwashangaza Australia baada ya kusawazisha bao hilo katika muda huo huo mfungaji akiwa ni Uchena Kanu na kuzifanya timu hizo ziende mapumziko zikiwa sare ya bao 1-1
Dakika ya 65 Nigeria waliandika bao la pili lililofungwa kwa kichwa na Osinachi Ohale kabla ya kuwashangaza Australia dakika saba baadaye walipoandika bao la tatu lililofungwa na Asisat Oshoala baada ya wachezaji wa Australia kujichanganya.
Pamoja na mabao hayo, Nigeria waliendelea kupambana lakini walikuwa ni Australia waliopata bao la pili lililofungwa na Alanna Kennedy.
Nigeria yenye pointi nne kama Canada Jumatatu itacheza na Nigeria wataumana na Jamhuri ya Ireland ambao kimsingi wameshaaga mashindano hayo yanayofanyika kwa ushirikiano katika nchi za New Zealand na Astralia.
Mafanikio makubwa ya timu ya Nigeria kwenye fainali za Kombe la Dunia za Wanawake ni yale ya mwaka 1999, timu hiyo ilipofikia hatua ya robo fainali.
Kombe la Dunia Nigeria yaibwaga Australia
Nigeria yaibwaga Australia
Read also