Na mwandishi wetu
Hesabu za Simba kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika sasa ni rasmi zimefikia tamati kwa msimu huu wa 2025-26 baada ya sare ya bao 1-1 na Petro Atletico ya Angola katika mechi iliyopigwa Jumamosi Februari 7, 2026.
Ile hadithi ya haiishi mpaka iishe, hatimaye imekwisha rasmi, Simba sasa itacheza mechi yake ya mwisho ya Kundi D dhidi ya Stade Malien kwa ajili ya kukamilisha ratiba za ligi hiyo.
Kabla ya mechi na Petro, Simba walikuwa wakijipa matumaini ya ushindi na kuwaombea njaa wapinzani wake wa kundi hilo lakini kwa sare yao na Petro nafasi hiyo haipo, sasa ni kujipanga kwa msimu ujao wa 2026-27.
Wakati Simba ikibaki mkiani na pointi zake mbili, Petro wao wamefikisha pointi sita na kushika nafasi ya tatu huku Stade Malien wakiendelea kushika usukani na pointi zao 11 na Esperance ya pili na pointi sitana timu hizo zitaumana Jumapili katika mechi nyingine ya kundi hilo.
Petro wakiwa nyumbani walianza mchezo kwa kasi na kupata bao la kuongoza katika dakika ya 13 mfungaji akiwa ni Pedro Pinto, bao ambalo lilidumu kwa dakika 45 za kwanza.
Zikiwa zimebakia dakika 10 kabla ya kutimia dakika 90, Simba walifanikiwa kupata bao la kusawazisha lililofungwa na Anicet Ora na kutuliza kelele za mashabiki wa Petro waliokuwa kwenye uwanja wa nyumbani.
Kimataifa Sare yaitoa rasmi Simba Ligi ya Mabingwa
Sare yaitoa rasmi Simba Ligi ya Mabingwa
Read also
