Na mwandishi wetu
Kiungo mshambuliaji wa Simba, Augustine Okrah amerejea kwenye maozezi ya kikosi hicho baada ya kukaa nje ya uwanja kwa takriban miezi miwili akisumbuliwa na jeraha la kidole.
Mchezaji huyo raia wa Ghana amerejea kwenye mazoezi ya kwanza ya timu hiyo tangu irejee nchini ikitoka Morocco ilikokwenda kucheza mechi yao ya mwisho ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Raja Casablanca na kupewa mapumziko ya siku mbili.
Okrah ambaye alipata jeraha hilo kwenye mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya Al Hilal ya Sudan mnamo Februari 5, mwaka huu, imemlazimu kukosa mechi za hatua ya makundi za Ligi ya Mabingwa.
Okrah hata hivyo anaweza kuukosa mchezo wa Kombe la FA (ASFC) dhidi ya Ihefu lakini inawezekana akawemo kwenye mechi ya Kariakoo Derby inayotarajia kupigwa Aprili 16, mwaka huu.
Soka Okrah aanza mazoezi Simba
Okrah aanza mazoezi Simba
Read also
