Na mwandishi wetu
Kipa wa Simba SC, Ali Salim amesema siri ya kiwango chake kuwa bora katika upanguaji wa penalti ni mbinu alizopewa na kocha wa makipa wa timu hiyo, Daniel Cadena.
Kipa huyo jana Jumatano alitoa mikwaju mitatu ya penalti ya wachezaji wa Singida Fountain Gate na kuiwezesha Simba kutinga fainali ya Kombe la Mapinduzi itakayochezwa keshokutwa dhidi ya mabingwa watetezi, Mlandege.
Akizungumza na GreenSports, kipa huyo alisema ulikuwa mchezo mgumu ndani ya dakika 90 ulioisha kwa sare ya 1-1 kutokana na ubora wa wapinzani wao Singida ambao waliingia katika mchezo huo kwa nguvu tangu mchezo ulipoanza.
“Siri kubwa ya ubora niliokuwa nao katika kupangua penalti ni kufanyia kazi mbinu ninazopewa na kocha wangu Cadena pamoja na juhudi zangu binafsi, namshukuru Mungu kwa kuisaidia timu yangu kufika fainali,” alisema Salim.
Alisema kwenye penalti anayepewa nafasi ya kufanya vizuri ni mpigaji, kipa asilimia zake ni chache inaweza kuwa 75 kwa 25 lakini yeye anapoingia kwenye penalti huwa hana wasiwasi wowote.
Alieleza kingine kilichomsaidia ni kujua vizuri uwezo wa wapigaji penalti hizo kama Gadiel Michael na Meddie Kagere ambao aliwahi kucheza nao Simba.
Soka Ali Salim amtaja kocha wa makipa Simba
Ali Salim amtaja kocha wa makipa Simba
Read also