London, England.
Winga wa Arsenal, Bukayo Saka wakati wowote kuanzia sasa anatarajia kusaini mkataba mpya na klabu hiyo inayoshika usukani kwenye Ligi Kuu England (EPL).
Mazungumzo kati ya Saka ambaye pia ni mchezaji wa timu ya Taifa ya England na vigogo wa Arsenal yanaendelea huku kukiwa na kila dalili za kufikia makubaliano ili mchezaji huyo aongeze mkataba.
Saka ambaye ndio kwanza ana miaka 21, kwa sasa ni mmoja wa wachezaji muhimu kwenye kikosi cha Arsenal kinachopigania taji la EPL akiwa tayari ameifungia timu hiyo mabao tisa na kutoa asisti 23.
Ni mchezaji aliyekulia katika akademi ya Arsenal na mkataba wake wa sasa unafikia ukomo mwaka 2024 huku ikidaiwa kwamba mkataba wake mpya na klabu hiyo utakuwa na thamani ya Pauni 10 milioni kwa mwaka.
Wanachotaka kufanya Arsenal ni kumpa mkataba utakaofikia ukomo mwaka 2028 ili waweze kuwa naye muda mrefu zaidi kuanzia sasa wakiwa wanafukuzia taji la kwanza kwa takriban miaka 19 iliyopita.
Saka akisaini mkataba huo atakuwa anaungana na kinda mwingine wa klabu hiyo ambaye pia ana miaka 21, Gabriel Martinelli wa Brazil ambaye mapema mwezi huu alisaini mkataba mpya Arsenal.
Kimataifa Saka kusaini mkataba mpya
Saka kusaini mkataba mpya
Read also