Na mwandishi wetu
Rasmi mshambuliaji wa FC Dallas ya Ligi Kuu Marekani, Benard Kamungo (pichani akiwa na Lionel Messi) amejumuishwa juzi kwa mara ya kwanza kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Marekani kwa vijana chini ya miaka 23.
Kamungo, 21 ambaye ni mzaliwa wa Kasulu, Kigoma ametajwa kwenye kikosi hicho cha awali kinachotarajia kushiriki Michezo ya Olimpiki itakayofanyika Ufaransa, mwakani.
Hiyo imekuja miezi michache tangu mchezaji huyo alipoitwa Juni, mwaka huu kuitumikia timu ya taifa ya Tanzania dhidi ya Algeria lakini alishindwa kutokana na sababu mbalimbali huku mwenyewe akieleza yuko tayari kuitumikia Tanzania kama mambo yatakaa sawa mapema.
Kamungo ambaye anafanya vizuri kwa sasa kwenye mechi za Ligi ya Marekani, aliondoka Kambi ya Nyarugusu, Kigoma na kuhamia Texas mwaka 2016 na familia yake kupitia Kamati ya Kimataifa ya Uokoaji (IRC) kabla ya kujiunga na North Texas mwaka 2021 kisha kutua Dallas mwaka jana.
Akiwa katika mazoezi na kikosi hicho kitakachocheza mechi za kirafiki dhidi ya Japan na Mexico, Kamungo anapaswa kuonesha uwezo wa juu ili kupata nafasi katika orodha ya mwisho ya kikosi kitakachoiwakilisha Marekani kwenye Michezo ya Olimpiki.
Kimataifa Kamungo aitwa timu ya taifa Marekani
Kamungo aitwa timu ya taifa Marekani
Read also