Na mwandishi wetu
Klabu za Kitayosce inayoshiriki Ligi Kuu NBC na Fountain Gate inayocheza Ligi ya Championship zimefungiwa kusajili wachezaji kwa msimu wa 2023/24.
Ofisa Habari na Mawasiliano wa Shirikisho la Soka (TFF), Cliford Ndimbo (Ndimbo) alisema uamuzi huo umefanywa na Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa) baada ya kocha Ahmed El Faramawy Yousef Mostafa Soliman kushinda kesi za madai yake dhidi ya klabu hizo.
“Kocha Soliman, raia wa Misri ambaye alizifundisha timu hizo kwa nyakati tofauti alifungua kesi Fifa akipinga kuvunjiwa mikataba kinyume cha taratibu. Baada ya kushinda kesi, klabu hizo zilitakiwa ziwe zimemlipa ndani ya siku 45 tangu uamuzi huo ulipotolewa, lakini hazikutekeleza hukumu hizo,” alisema Ndimbo.
Ndimbo pia alifafanua kuwa wakati Fifa imezifungia klabu hizo kufanya uhamisho wa wachezaji kimataifa, TFF yenyewe imezifungia kufanya uhamisho wa ndani.
“TFF inazikumbusha klabu kuheshimu mikataba ambayo zimeingia na wachezaji pamoja na makocha ili kuepuka adhabu mbalimbali ikiwemo kufungiwa kusajili na iwapo klabu inataka kuvunja mkataba na mchezaji au kocha, inatakiwa kufanya hivyo kwa kuzingatia taratibu,” aliongeza Ndimbo.
Soka Fifa yashusha rungu Kitayosce, Fountain Gate
Fifa yashusha rungu Kitayosce, Fountain Gate
Read also