Na mwandishi wetu
Timu ya Singida Fountain Gate imepanga kuendeleza makali yake katika michuano ya Kombe la Mapinduzi kwa kuhakikisha inatwaa ubingwa wa michuano hiyo msimu huu.
Singida ambayo msimu uliopita ilifungwa kwenye fainali ya michuano hiyo na Mlandege mabao 2-1 ni miongoni mwa timu nne zinazoiwakilisha Tanzania Bara kuelekea michuano hiyo.
Michuano ya kila mwaka ya Kombe la Mapinduzi itaanza kuunguruma Januari mwakani ambapo mbali na Singida FG, timu nyingine za Tanzania Bara zitakazoshiriki michuano hiyo ni Azam FC, Simba na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu NBC, Yanga.
Ofisa Habari wa Singida, Hussein Masanza (pichani) ameiambia GreenSports kuwa wanaingia kwenye kombe hilo wakiamini huu ni wakati wao mwingine kudhihirisha kuwa wanaweza kutwaa kombe hilo licha ya kuwa wageni katika ushiriki.
“Msimu uliopita ilikuwa ni mara yetu ya kwanza kushiriki na tukafika fainali, safari hii tunataka kucheza fainali nyingine na kubeba kombe.
“Ni muhimu zaidi kwa timu kama yetu kuchukua makombe haya maana yanatupa motisha ya kupambania zaidi makombe mengine makubwa tunayoshiriki kwa sasa ikiwemo ligi kuu, hivyo tumedhamiria na tunaamini tunakwenda kufanya hivyo,” alisema Masanza.
Timu nyingine zitakazoshiriki msimu huu ni bingwa mtetezi, Mlandege, KVZ, Chipukizi na Jamhuri kutoka Zanzibar pamoja na Vital’O ya Burundi, APR (Rwanda), Bandari (Kenya) na URA ya Uganda.
Soka Singida FG yalitaka taji la Mapinduzi
Singida FG yalitaka taji la Mapinduzi
Read also