Doha, Qatar
Kocha wa timu ya Taifa ya Uholanzi, Louis van Gaal amesifia maandalizi na miundombinu ya Qatar kwa ajili ya fainali za Kombe la Dunia ingawa amehoji uamuzi wa kuifanya nchi hiyo kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa.
Akifafanua kuhusu kauli yake hiyo, Van Gaal amesema kwamba Qatar ni nchi ndogo mno kuandaa mashindano hayo na haina historia kubwa kwenye soka na awali aliwahi kunukuliwa akisema kwamba uamuzi wa kuipa nchi hiyo fainali hizo ni jambo lisilo na mantiki.
“Lengo la Fifa ilikuwa ni kuziendeleza nchi na kwa hiyo tunacheza hapa lakini nchi za soka zina uzoefu na kila kitu na hapo hapo unaweza kuzihamasisha nchi nyingine katika namna nyingine ambayo ni sahihi,” alisema kocha huyo mwenye umri wa miaka 71.
Kocha huyo pia alisema kwamba baadhi ya marafiki zake na ndugu wa familia walipata tabu kufanya ‘booking’ kwenye mahoteli kwa ajili ya fainali hizo ambazo zinaanza rasmi Jumapili hii katika nchi hiyo ambayo ina watu wasiozidi milioni tatu na viwanja vinane kwa ajili ya mechi za michuano hiyo.
“Lakini kwa upande wa maandalizi na viwanja na kila kitu ikiwamo miundombinu ni mambo yaliyo vizuri,” alisema kocha huyo ambaye nchi yake licha ya kuwa miongoni mwa mataifa makubwa katika ulimwengu wa soka lakini ilishindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka 2018 zilizofanyika nchini Urusi.
Kimataifa Van Gaal aipongeza, aikataa Qatar
Van Gaal aipongeza, aikataa Qatar
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
