London, England
Beki wa Chelsea na timu ya Taifa ya Senegal, Kalidou Koulibaly ametimkia Saudi Arabia akiwa tayari amekamilisha usajili wa kujiunga na klabu ya Al-Hilal.
Koulibaly ambaye ni beki wa kati, ni staa mwingine wa Ulaya kuhamia Saudi Arabia akitanguliwa na nyota mwenzake waliyekuwa naye Chelsea kiungo, N’Golo Kante ambaye pia amejiunga na Al-Ittihad.
Mchezaji mwingine ambaye hivi karibuni alitimkia Saudi Arabia ni Ruben Neves wa Wolves ambaye amesaini mkataba wenye thamani ya Pauni 47 milioni na Al-Hilal kama ilivyo kwa Koulibaly.
Habari zaidi zinadai kwamba beki wa Man City, Eduardo Mendy ambaye hivi karibuni aliingia matatani akituhumiwa kubaka na kudhalilisha wasichana, naye yuko njiani kuelekea Saudi Arabia.
Koulibaly ambaye alijiunga na Chelsea Julai mwaka jana kwa mkataba wa miaka minne akitokea Napoli ya Italia, mwaka jana aliiwezesha Senegal kubeba Kombe la Mataifa ya Afrika wakati akiwa na Napoli mwaka 2020 aliiwezesha timu hiyo kubeba taji la Italia.
Akiwa Chelsea amecheza jumla ya mechi 32 za mashindano yote na kufunga mabao mawili katika mechi 23 za Ligi Kuu England (EPL).
Januari mwaka huu Cristiano Ronaldo aliihama Man United na kujiunga na klabu ya Al Nassr ya Saudi Arabia na katika mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni alisema anaamini wachezaji wenzake wengi watamfuata Saudi Arabia.
Kimataifa Koulibaly atimkia Saudi Arabia
Koulibaly atimkia Saudi Arabia
Read also