Na mwandishi wetu
Kocha mpya wa timu ya Kagera Sugar, Mecky Maxime ameeleza kuwa ametua katika kikosi hicho kwa ajili ya kuwapa ushindi mashabiki wa Kagera na si vinginevyo.
Maxime amerejea kwa mara ya pili kuinoa timu hiyo akirithi mikoba ya Mkenya, Francis Baraza aliyevunjiwa mkataba wake hivi karibuni kutokana na matokeo mabovu ya timu hiyo tangu kuanza kwa msimu huu.
Kocha huyo alisema hana kikubwa cha kuwaahidi mashabiki wa Kagera zaidi ya kufanya kazi na kutafuta ushindi kwani anafahamu kama hakuna ushindi si maneno yatakayomuokoa katika kufukuzwa kazi.
“Matokeo ni majaliwa ya Mungu kama vile watu wanapotafuta pesa, huyu anapata nyingi huyu anakosa, hakuna cha kuzungumza, watu wanataka ushindi kama hakuna ushindi wanakuondoa, mtu anapokupa kazi anataka matokeo.
“Kikubwa mimi ni mwalimu wa mpira, nitafanya ninavyofahamu mimi, kuingiza mbinu zangu na kufikia malengo ambayo ni ushindi, siwezi kuwa na sababu nyingi za kwamba sijasajili hii timu au vipi, ukisema hivyo maana yake umeanza kufeli mapema,” alisema Maxime.
Maxime anatarajiwa kuanza kazi rasmi leo katika mechi dhidi ya KMC, mchezo unaopigwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.
Soka Maxime ataja kilichompeleka Kagera
Maxime ataja kilichompeleka Kagera
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
