Na mwandishi wetu
Bao la kujifunga na Ruvu Shooting limetosha kuifanya Yanga izidi kujiimarisha kileleni baada ya kuvuna pointi tatu muhimu kupitia bao hilo pekee katika mechi ya Ligi Kuu NBC.
Katika mechi hiyo iliyopigwa Jumatatu hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar es Salaam, bao hilo pekee katika mchezo huo lilitokana na makosa ya beki wa Ruvu, Mpoki Mwakinyuke katika dakika ya 17 mchezo huo.
Mwakinyuke beki wa kushoto wa Ruvu, alijikuta katika majanga hayo wakati akijaribu kuokoa hatari langoni mwake lakini akashindwa kufanya alichodhamiria na kujikuta akiiachia majanga timu yake.
Kwa ushindi huo Yanga inazidi kuikimbia Simba katika kuwania taji la ligi hiyo ikiwa imefikisha pointi 56 na kuiacha Simba inayoshika nafasi ya pili kwa tofauti ya pointi sita huku timu zote zikiwa zimecheza mechi 21 hadi sasa.
Matokeo hayo pamoja na kuipa Yanga pointi lakini yanaacha swali hasa kwa namna ambavyo ushindi huo umepatikana dhidi ya timu ya Ruvu ambayo inashika mkia ikiwa na pointi 14 tu katika mechi 21.
Kinachoonekana sasa ni kwamba Yanga ina kazi ya kusahihisha makosa katika mechi tisa zilizobaki ili iweze kuitimiza nia yake ya kulitetea taji la ligi baada ya kushindwa kuonyesha ubora dhidi ya Ruvu, timu ambayo katika mechi zake 21 imeshinda tatu tu na kutoka sare mara tano na bado kidogo iongeze sare ya sita katika mechi yake na Yanga.
Nayo Azam inabaki katika nafasi ya tatu ikiwa na pointi 43 baada ya jana kupoteza mchezo wake mbele ya Singida Big kwa kuchapwa bao 1-0. Timu hizo zote zimecheza mechi 21 na kila moja ina pointi 43 zikizidiana kwa wastani wa mabao ya kufunga na kufungwa.
Ligi hiyo itaendelea leo Jumanne kwa mechi mbili…
KMC vs Namungo
Geita Gold vs Coastal Union
Soka Bao la kujifunga laibeba Yanga
Bao la kujifunga laibeba Yanga
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
