Manchester, England
Kocha wa Man United, Erik Ten Hag amempongeza mchezaji wake, Marcus Rashford kwa kufunga mabao mawili yaliyoiwezesha timu hiyo kupata ushindi wa mabao 3-2 katika mechi ya Europa Ligi dhidi ya Omonia Nicosia.
Katika mechi hiyo iliyochezwa Alhamisi usiku, Rashford ambaye aliingia akitokea benchi, licha ya kufunga mabao mawili ndiye aliyemchezesha Antony Martial ambaye alifunga bao la pili kwa timu hiyo na hatimaye kupata ushindi ugenini.
“Nafikiri wachezaji wa akiba walikuwa na faida kubwa leo na hilo ni jambo zuri, hilo linaonyesha uimara wa timu,” alisema Ten Hag.
Awali Nicosia waliibua mshtuko walipopata bao la kwanza katika dakika ya 34 lililofungwa na Karim Ansarifard hali iliyowafanya Man United kupambana kusawazisha lakini haikuwezekana hadi timu zinakwenda mapumziko.
Dakika nane baada ya mapumziko, Rashford akiwa ndio kwanza ameingia uwanjani baada ya kipindi cha pili tu kuanza akichukua nafasi ya Sancho, aliwainua vitini mashabiki wa Man United baada ya kusawazisha bao hilo.
Martial naye aliandika bao la pili katika dakika ya 63 akiitumia vizuri pasi ya Rashford, Martial alifunga bao hilo dakika moja tu baada ya kuingia uwanjani akichukua nafasi ya Bruno Fernandes.
Rashford akakamilisha ushindi wa Man United katika dakika ya 84 akiitumia pasi ya Cristiano Ronaldo ambaye katika mechi hiyo Ten Hag alimpanga kuanzia kipindi cha kwanza. Nicosia licha ya kufungwa mabao hayo mawili walipambana na kupata bao la pili dakika ya 85 lililofungwa na Nikolas Panagiotou.
Matokeo ya mechi za Alhamisi za Europa Ligi…
Malmö 0-1 Union Berlin
Omonia Nicosia 2-3 Man Utd
Arsenal 3-0 Bodo
Zürich 1-5 PSV Eindhoven
HJK Helsinki 1-1 Ludogorets
Sheriff Tiraspol 0-2 Real Sociedad
Sturm Graz 0-0 Lazio
Red Star 4- 1 Ferencvarosi
Monaco 3-1 Trabzonspor
Fenerbahce 2-0 AEK Larnaca
Rennes 2-1 Dynamo Kyiv
Roma 1-2 Real Betis
Kimataifa Ten Hag ampongeza Rashford
Ten Hag ampongeza Rashford
Green SportsAuthor / Greensports Media LTD
Greensports author
Read also
