Manchester, England
Baada ya kuifungia Man City mabao matano katika ushindi wa 6-2 dhidi ya Luton kwenye Kombe la FA wiki iliyopita, mshambuliaji wa Man City, Erling Haaland amesema bado ana nafasi ya kuboresha kiwango chake zaidi.
Haaland ambaye msimu uliopita aliifungia Man City mabao 80 katika mechi 84, ametoa kauli hiyo wakati City ikijiandaa kuumana na FC Copenhagen katika mechi ya pili ya hatua ya mtoano (16 bora) ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Katika mechi ya kwanza baina ya timu hizo, Man City ilitoka uwanjani na ushindi wa mabao 3-1 na mechi ya leo huenda ikawa nafasi nyingine kwa Haaland kuonesha ubora katika kuzifumania nyavu.
Msimu uliopita Haaland aliibuka mfungaji bora wa Ligi Kuu England (EPL) na mabao yake yalichangia Man City kubeba mataji matatu ya EPL, Ligi ya Mabingwa Ulaya na FA.
Haaland, 23, hadi sasa ndiye kinara wa mabao kwa msimu huu licha ya kukosa mechi kadhaa kwa kipindi cha zaidi ya mwezi mmoja kutokana na kuwa majeruhi.
Pamoja na kufunga bao Jumapili dhidi ya mahasimu wao wa jiji la Manchester, Man United, Haaland bado anakumbuka alivyokosa bao la wazi akiwa yeye na goli jambo ambalo analitaja kuwa ni ushahidi wa kwa nini bado ana kazi ya kufanya bidii ili awe bora zaidi.
“Kuna mengi ya kufanya ili niwe bora, watu wanasema niko vizuri kwenye kufunga mabao lakini nilipoteza nafasi ya wazi kuwahi kutokea duniani, hivyo nami natakiwa kuwa bora katika eneo hilo,” alisema Haaland.
Haaland anasema kwamba jambo hilo linabaki kuwa changamoto kwake hasa anapokumbuka wakati akiwa mdogo wakati ambao alikuwa akishindwa kufunga bao nafasi ya wazi alikuwa akilia na kwa sasa analifanyia kazi jambo hilo la kukosa nafasi za wazi.
Man City kwa sasa inapambana kuweka historia mpya ya kuwa timu ya kwanza kubeba taji la EPL mara nne mfululizo.
Mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya leo Jumatano
Man City v FC Copenhagen
Real Madrid v RB Leipzig
Kimataifa Haaland hajaridhika na ubora wake
Haaland hajaridhika na ubora wake
Read also