Mainz, Ujerumani
Winga wa Mainz 05 ya Ujerumani, Anwar El Ghazi (pichani) amezuia kufanya mazoezi na kucheza mechi za timu hiyo baada ya kuweka kwenye mitandao ya kijamii andiko kuhusu vita ya Israel na Palestina.
El Ghazi, 28, hata hivyo baadaye alifuta andiko hilo ambalo klabu yake haikukubaliana nalo na ndio maana ikamchukulia hatua nyota huyo wa zamani wa Aston Villa na Everton ambaye alijiunga na timu hiyo akiwa mchezaji huru.
Katika taarifa ya kumsimamisha mchezaji huyo kutoka Uholanzi, klabu ya Mainz ilieleza, ”Kabla ya kuchukua uamuzi klabu na mchezaji tulifanya mazungumzo ya kina.”
“Mainz 05 inaheshimu ukweli kwamba kuna mtazamo wa pande mbili katika mgogoro huu wa Mashariki ya Kati kwa zaidi ya miaka 10 sasa,” ilieleza taarifa hiyo.
“Hata hivyo klabu inajitenga na maandiko ya kwenye mitandao ya kijamii kuhusu jambo hilo kwa sababu haiendani na msimamo wa maadili ya klabu,” ilifafanua taarifa hiyo.
Katika hatua nyingine klabu ya Bayern Munich nayo inadaiwa kujiandaa kufanya kikao na beki wake, Noussair Mazraoui, baada ya beki huyo kutoka nchini Morocco kuonesha video ya mgogoro huo kupitia mtandao wa Instagram.
Naye beki wa Nice ya Ufaransa, Youcef Atal anachunguzwa na waendesha mashitaka nchini Ufaransa akidaiwa kuweka kwenye mitandao ya kijamii video inayohusu mgogoro huo.
Kimataifa Mgogoro Israel, Palestina wamtia matatani mchezaji
Mgogoro Israel, Palestina wamtia matatani mchezaji
Read also