Na mwandishi wetu
Benki ya NMB imetoa zaidi ya Sh milioni 200 kwa ajili ya zawadi za mashindano ya Kombe la Mapinduzi, Zanzibar na ‘traki-suti’ 150 kwa ajili ya kuvaa kwenye matembezi Siku ya Mapinduzi.
Fedha hizo kwa ajili ya bingwa ambaye atazoa Sh milioni 100 /, timu itakayoshika nafasi ya pili Sh milioni 70, pamoja na medali za mabingwa na mshindi wa pili.
Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi nguo za mazoezi kwa ajili ya siku ya mazoezi kitaifa yatakayofanyika Januari Mosi, mwakani, Meneja Biashara Zanzibar wa NMB, Naima Said Shaame alisema udhamini huo unalenga azma ya benki ya NMB na pia juhudi za serikali katika kusherehekea miaka 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar.
‘’Kama benki tunasema huu sio mwisho wa udhamini wetu. Tunaamini michezo sio tu inachangia ustawi wetu, lakini pia inatuleta pamoja kama taifa,” alisema.
Akizungumza baada ya kupokea vifaa hivyo, Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Zanzibar, Fatma Hamad Rajab, aliishukuru NMB kwa misaada mbalimbali inayotoa.
Alisema benki hiyo ni kiongozi wa kutoa misaada kwa serikali katika nyanja zote za michezo na jamii, hivyo msaada huo umekuja wakati muafaka kwani siku ya mazoezi ya kitafa ni siku kubwa.
Fatma alisema amepokea misaada hiyo kwa furaha, ambapo ameitaka benki hiyo kuendelea kusaidia kwani bado kuna mahitaji mengi yanatakiwa ili kuendeleza michezo Zanzibar.
Sports Mix NMB yatoa milioni 200 Kombe la Mapinduzi
NMB yatoa milioni 200 Kombe la Mapinduzi
Read also