Madrid, Hispania
Klabu ya Real Madrid imekamilisha usajili wa kiungo mwenye umri wa miaka 18, Arda Guler au Messi wa Uturuki kutoka klabu ya Fenerbahce ya Uturuki.
Kinda huyo amesaini mkataba wa miaka sita ambapo sasa ataungana na mchezaji mwingine wa kiungo aliyesajiliwa na klabu hiyo hivi karibuni, Jude Bellingham ambaye ana miaka 19.
Katika msimu uliopita, Guler aliifungia Fenerbahce mabao manne na kutoa asisti nne na kuwa nyota wa mchezo katika mechi ya fainali ya Kombe la Uturuki.
Hadi kumpata mchezaji huyo, Real Madrid ilikuwa ikichuana na klabu za Arsenal, Man United na Newcastle za England pamoja na PSG ya Ufaransa na Bayern Munich ya Ujerumani ingawa pia kulikuwa na habari kwamba Barca nao walikuwa wakimuwinda.
Real Madrid hata hivyo haikuweka wazi ada ya uhamisho ya mchezaji huyo ambaye alianza kutamba na Fenerbahce akiwa na miaka 16, ingawa inakisiwa kwamba ada yake inaweza kuwa Euro 20 milioni.
Ukiacha Bellingham, wachezaji wengine wa Real Madrid makinda ambao wamesajiliwa miaka ya karibuni ni Rodrygo, Eduardo Camavinga, Vinicius Jr na Aurelien Tchouameni.
Kimataifa Messi wa Uturuki asaini Real Madrid
Messi wa Uturuki asaini Real Madrid
Related posts
Read also
