Munich, Ujerumani
Klabu ya Chelsea inadaiwa kufanya mazungumzo na kocha wa zamani wa Bayern Munich, Julian Nagelsmann ili akabidhiwe mikoba ya kuinoa timu hiyo inayochechemea kwenye Ligi Kuu England.
Kwa sasa timu hiyo inanolewa na kocha wa muda, Frank Lampard ambaye naye mambo hayaonekani kuwa mazuri huku mabosi wa timu hiyo wakianza kuwekeza nguvu kwa ajili ya msimu ujao.
Katika hesabu za msimu ujao, moja ya kazi kubwa inayofanywa ni kumtafuta kocha atakayekabidhiwa mikoba ya kuinoa timu hiyo huku jina la Nagelsmann (pichani) likionekana kupewa nafasi kubwa.
Chelsea hivi karibuni ilimtimua kocha Graham Potter baada ya mambo kumuendea kombo. Potter alichukua jukumu la kuinoa timu hiyo kutoka kwa Thomas Tuchel ambaye naye alitimuliwa na kwa sasa anainoa Bayern Munich.
Iwapo Chelsea watafanikiwa kumchukua Nagelsmann, kocha huyo atakuwa kama amebadilishana timu na Tuchel ambaye kwa sasa anainoa Bayern timu iliyomtimua Nagelsmann hivi karibuni.
Kocha mwingine ambaye amekuwa akihusishwa na Chelsea, ni kocha wa zamani wa Barca, Luis Enrique ambaye amekuwa hana kazi tangu aachane na timu ya Taifa ya Hispania baada ya fainali za Kombe la Dunia za Qatar.
Kimataifa Chelsea, Nagelsmann wateta
Chelsea, Nagelsmann wateta
Read also